Shirika la Waandishi wa lugha ya Kiswahili (SHIWAKI) liliandaa Tamasha la Waandishi wa Kiswahili ambalo lilihudguriwa na wadau mbalimbali na wapenzi wa fasihi ya Kiswahili. Tukio hili lilifanyika tarehe 16 Agosti 2026 katika ukumbi wa Alliance Francais, Nyali, Mombasa.

Tamasha hili lilikuwa ni mahsusi kuwapongeza na kuwatuza washindi wa tuzo ya Kiswahili ya Safal ya fasihi ya Afrika kwa mwaka 2024 katika nyanja zote. Washindi waliweza kusoma na kuelezea kwa uchache sehem ya kazi zao zilizoshinda na kujibu maswali kadhaa kutoka kwa hadhira.

Kabla ya hafla ya ukumbini, kulikuwa na kipindi cha redio majira ya asubuhi kilichoendeshwa mubashara katika studio za Swahilipot FM.

Categorized in: