Nasaha
” Jipende, jisheue, jilee, jienue, jifurahishe. Hakuna atakayekufanyia hayo zaidi ya wewe mwenyewe. “
Fatma Shafii
“Mwanangu mpendwa, thamani ya macho yangu na tabasamu la moyo wangu. Sikiza yale nikwambiayo; malezi yangu kwako ni ufunguo tosha wa kufanikiwa katika maisha yako. Sina mali mengi ya kukurithisha au kukunufaisha. Urithi wangu juu yako ni yale uliosoma na kuiga kutoka kwangu. Elimu uliochuma kwangu ni matunda na urithi kwako. Penda unapopendwa na mpende zaidi anayekuchukia. Chunga na tathmini… “
Hamdan Mohamed
” MALIMWENGU Waama, dunia huleta mema na mawi. Binadamu hujiwa na mambo mazuri na mabaya. Mithili ya shilingi ina pande mbili. Naam! Hii ndiyo falsafa ya maisha. Kamwe hayatabiriki. Malimwengu yatokea bila ratiba au mpangilio wowote. Sisi wenyewe hatujui kesho yetu itakuwa vipi? Japo tuna imani na matumaini kutapambazuka vyema. Maishani tunakumbana na changamoto, misukosuko, balaa kila nui. Mawimbi yavumapo hatuna… “
Kassim Kombe
” Katika maisha kuna mengi sana yanatokea ila hatujui maana yake wala sababu zake, ila kwa hali ya kibinadam huwa tunapenda kulalamika na kuhuzunika na kuwalaumu waliotutendea AU waliotusababishia katika kitabu kitukufu cha Quran kuna sura moja inaitwa surat al kahf ni sura ya 18 .. Maana yake kwa kiswahili ni pango.. Kwa Imani ya dini ya kiislam kuna swawabu nyingi… “
Amiry
“Usikitamani kitu fulani sana, wakati mwingine kutamani kitu sana huondoa bahati kwenye kitu hicho…” The Pearl “
Paul Nganga
” Wahenga watujuza,”Kauli nzuri ni ridhaa ya mtima.” Tujitahidi kuongea maneno yenye tija wala sio kubwabwaja. “
Kassim Kombe
” Kila safari ni hatua.. “
Martin
” Urafiki ni siri. Tuhifadhi ya wandani wetu bila kuyaanika hadharani. “
Kassim Kombe
- 1
- 2
