Mashairi

Hadithi

Nasaha

Jipende

” Jipende, jisheue, jilee, jienue, jifurahishe. Hakuna atakayekufanyia hayo zaidi ya wewe mwenyewe. “

Fatma Shafii

Nasaha kutoka kwa mamangu mpendwa.

“Mwanangu mpendwa, thamani ya macho yangu na tabasamu la moyo wangu. Sikiza yale nikwambiayo; malezi yangu kwako ni ufunguo tosha wa kufanikiwa katika maisha yako. Sina mali mengi ya kukurithisha au kukunufaisha. Urithi wangu juu yako ni yale uliosoma na kuiga kutoka kwangu. Elimu uliochuma kwangu ni matunda na urithi kwako. Penda unapopendwa na mpende zaidi anayekuchukia. Chunga na tathmini… “

Hamdan Mohamed

Kassim Kombe ( malenga mpambe)

” MALIMWENGU Waama, dunia huleta mema na mawi. Binadamu hujiwa na mambo mazuri na mabaya. Mithili ya shilingi ina pande mbili. Naam! Hii ndiyo falsafa ya maisha. Kamwe hayatabiriki. Malimwengu yatokea bila ratiba au mpangilio wowote. Sisi wenyewe hatujui kesho yetu itakuwa vipi? Japo tuna imani na matumaini kutapambazuka vyema. Maishani tunakumbana na changamoto, misukosuko, balaa kila nui. Mawimbi yavumapo hatuna… “

Kassim Kombe

Nasaha Toka Bandari Salama(Dar es Salaam)

” Katika maisha kuna mengi sana yanatokea ila hatujui maana yake wala sababu zake, ila kwa hali ya kibinadam huwa tunapenda kulalamika na kuhuzunika na kuwalaumu waliotutendea AU waliotusababishia katika kitabu kitukufu cha Quran kuna sura moja inaitwa surat al kahf ni sura ya 18 .. Maana yake kwa kiswahili ni pango.. Kwa Imani ya dini ya kiislam kuna swawabu nyingi… “

Amiry

John Steinbeck

“Usikitamani kitu fulani sana, wakati mwingine kutamani kitu sana huondoa bahati kwenye kitu hicho…” The Pearl “

Paul Nganga

Kassim Kombe

” Wahenga watujuza,”Kauli nzuri ni ridhaa ya mtima.” Tujitahidi kuongea maneno yenye tija wala sio kubwabwaja. “

Kassim Kombe

Hassan Ali Kauleni

” Kila safari ni hatua.. “

Martin

Kassim Kombe

” Urafiki ni siri. Tuhifadhi ya wandani wetu bila kuyaanika hadharani. “

Kassim Kombe

Methali..

“Chui hakumbatiwi.”

Martin

Kassim Kombe

“Rasharasha ndio mwanzo wa mvua.” Ufanisi hupatikani siku moja. “

Kassim Kombe

Msheshe.R.Rashid

” Wali wa kushibia huonekana siniani . “

Msheshe . R . Rashid

Asiyejulikana

” Haijalishi kama wewe ndio mwindaji au awindwaye, lakini jua lituapo, afadhali ukimbilie usalama wako. “

Paul Nganga