Si hasha tuvimbiane, kwa maneno ya kuuma, fojo zikatwelemea
Ni wazi tuambiane, pendo halipo salama, kidete lachechemea
Ukitaka tuachane, nambie bado mapema, mapenzi hayajamea
Mi sitaki tugombane, niache bila hujuma, nijuwe pa kuhamia
Ukweli usiubane, ukanidhili kwa homa, kutwa kukufikiria
Kumbe unae mwengine, ambako moyo wapuma,
kwangu unapita njia
Othman Ame Hamza
Mfungwa huru
Chumbuni, Unguja-Zanzibar
0776820608
othame10@gmail.com
Alhamis 9/9/2021
WRITER – OTHMAN HAMZA