Yule niliyempenda, moyoni nikamuweka
Ananifanyia inda, leo amenigeuka
Kimoyo kinanidunda, mapigo yahisabika
Moyoni nina kidonda, kidonda kisotibika.

Umesalitika moyo, moyo unasulubika
Haupati utakayo, zaidi ya patashika
Aloushika hanayo, dharau kila dakika
Moyoni nina kidonda, kidonda kisotibika.

Othman Ame Hamza
Mfungwa huru
Chumbuni, Unguja-Zanzibar
+255 776 820 608
othame10@gmail.com

WRITER – OTHMAN HAMZA

Categorized in: