Furaha iliyoje kwetu sisi wazungumzaji wa lugha wa Kiswahili! Umoja wa Afrika (AU) umeipitisha lugha ya Kiswahili kuwa lugha rasmi ya kikazi itakayotumika ndani ya shughuli za umoja huo. Ifahamike kuwa Umoja wa Afrika ni muungano wa mataifa 54 yanayopatikana barani Afrika.

Jambo hili limekuja baada ya ombi la Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Bw. Philip Mpango kukubaliwa. Bw. Philip Mpango alisema ya kwamba Kiswahili ni lugha inayokadiriwa kutumiwa na zaidi ya watu milioni 100 wanaopatikana ndani na nje ya Afrika.

Ikumbukwe pia, mnamo mwezi Novemba Umoja wa Mataifa uliipitisha tarehe 7 Julai kuwa siku ya Lugha ya Kiswahili ulimwenguni.

Tunafurahia kwa kweli kwa kushuhudia hatua ambazo lugha hii zinazochukua. Panajo majaaliwa ipo siku tutafika tunapostahili kuwa!Kiswahili kitukuzwe! 

Categorized in: