Mwishoni mwa mwezi Machi 2023, waandaaji wa TUZO YA KISWAHILI YA SAFAL-CORNELL YA FASIHI YA AFRIKA walitangaza rasmi kupitia tovuti yao juu ya kufunguliwa pazia la ushiriki kwa msimu wa 8 wa tuzo hii.
Tuzo hii iliyoanzishwa mwaka wa 2014 ni mojawapo wa tuzo kubwa zinazoongoza katika kukitukuza na kukienzi Kiswahili na fasihi ya Afrika kwa jumla.
Miswada yote inastahili kuwasilishwa kwa lugha Kiswahili na mwisho wa kutuma miswada ni tarehe 30 Juni 2023.
Ukiwa una nia thabiti ya kuwasilisha mswada wako, fuatilia uzi ulioko hapa chini kupata maelekezo zaidi ya namna ya kushiriki.
