Karibuni marafiki, watunzi na wahariri
Sote tuweze shiriki, kutunga tungo mahiri
Tuungane na shiwaki, fasihi tuikariri
Tuweze pia hakiki, hadithi na mashairi

Tutunge kila wakati, kwa ladha za kuvutia
Mchana na lailati, nakala kuzipitia
Zisomeke zetu hati, nyoyo zipate tulia
Mbele ya kila umati, wasome kufurahia

Alhamdan Mohamed Kalamu Dumu Daima

Categorized in: