Lugha ni mali jamani, chombo kilicho muhimu
Lugha huleta amani, kwetu sisi wanadamu
Lugha tuipe thamani, ni funguo za elimu
Hutumika maishani , mambo yote kufahamu

Lugha ni yetu asili, pia ni kitambulisho
Lugha hasa Kiswahili, ina tele mafundisho
Lugha ni kiwiliwili, cha kuleta suluhisho
Lugha ni picha kamili, maneno kwa ufupisho

Alhamdan Mohamed
Kalamu Dumu Daima

Categorized in: