Mazingira ni jumla ya mambo yote yanayomzunguka kiumbe katika maisha yake. Kwa hiyo kila unachokiona ni mazingira yako. Katika gatuzi dogo la Likoni kaunti ya Mombasa, kuna vijana kwa jina la Musoma Youth Group. Ni mojawapo wa kikundi cha kupigiwa mfano kwa kujitolea kuzoa taka katika eneo hilo na kuhakikisha usafi wa mazingira ungalipo. Licha ya hivyo, wanakumbwa na changamoto ainati mathalan kukosa glavu wanapokusanya takataka na kuziweka katika mapipa. Ni ombi langu kwa mashirika ya kibinafsi na yasiyo ya kiserikali kuwajibika vilivyo kuhakikisha usafi umedumishwa. Kongole kedekede kwa vijana hao wa Mombasa.
Martin Mwendwa Mwanthi, Tubonge Youth initiative-Likoni,Mombasa

WRITER – Martin

Categorized in: