Nammininia sifa kedekede mwanahabari Mkalla Mwambodze wa kituo cha Radio Citizen, kwa kazi kuntu anayofanya ya kuwafikia na kuangazia talanta na kazi murwa inayofanywa na vijana mashinani bila kulazimishwa.Ni furaha isiyo na kifani haswa anapoangazia katika ukurasa wake wa facebook mambo mazuri ya kupigiwa mfano na wanahabari wengine katika tasnia ya utangazaji haswa michezo.Hivi majuzi majuzi aliangazia talanta katika kaunti ya Mombasa-Likoni na viongozi wenye umri mdogo waliojitolea kwa hali na mali kuhubiri AMANI katika kaunti ndogo ya LIKONI. Wanahabari tuige mfano wake tutambue talanta mashinani pasi na kupendelea adinasi yeyote.Kongole furifuri Mkalla mwambodze!!
MARTIN MWENDWA MWANTHI, TUBONGE YOUTH INITIATIVE-LIKONI MSA.

WRITER – MARTIN

Categorized in: