Hivi majuzi gatuzi dogo la Mvita huko Mombasa lilishuhudia moto mkubwa ambapo umewaacha wengi kupigwa na butwaa pasi na kuelewa chanzo chake. Ni dhahiri shahiri Mikasa ya moto imekuwa ikileta hasara Kwa biashara,maafa na kupoteza vitu ainati vyenye thamani kuu.Suluhi Iko wapi? Aidha,ni lazima kama ibada serikali za kaunti kuwa na mikakati mbadala ili kupambana na Mikasa kama ii hii siku za usoni. Sharti wananchi wahamasishwe dhidi ya kujikinga na moto.La sivyo,tutazidi kuuma vidole huku hasara kubwa ikitukodolea macho.Aidha,sharti vitengo vyote husika katika idara hiyo ziwajibike.
Martin Mwendwa Mwanthi, Tubonge Youth initiative-Likoni,Mombasa

WRITER – MARTIN

Categorized in: