Mzalendo wa ukweli, ni yule ambaye kwamba
Hutunza hali na mali, nchi yake huipamba
Yeye huwa ni mkali, kwa wale wanoichamba
Huwafukuza fahali, mamba wanaojigamba

Mzalendo alo bora, huilinda nchi yake
Mali huacha kupora, huchukuwa fungu lake
Hana visa vya kikora, hasaliti watu wake
Yeye ni mtu imara, hujenga taifa lake

Huipenda nchi yake, moyoni huithamini
Upendo aina yake, wa amani na imani
Huhamasisha wenzake, uzalendo maishani
Hakuna mfano wake, kama si wewe ni nani?

Alhamdan Mohamed
Kalamu Dumu Daima.

WRITER – HAMDHAN MOHAMED

Categorized in: