Kalamu naiijua, kwa idhini ya Rabuka,
Kulisifu langu ua, moyo wangu liloteka,
Lenyewe linatambua, kwake mimi nimefika.

Ni jingi la upole, ukarimu na nidhamu,
Halinyoshei kidole, yoyote binadamu,
Hizi sifa ni za kale, kupata sasa adimu.

Abu Junaid Suleiman

Categorized in: