Jukwaa la kimataifa linalojihusisha na masuala ya fasihi na utamaduni katika kueneza ujumbe wa amani duniani (IFLAC), limefungua dirisha la kupokea mawasilisho ya kazi za ushairi zinazohamasisha amani katika lugha ya Kiswahili, Kingereza, Kifaransa, Kiyahudi, Kireno na Kispanyola.

Mawasilisho ya kazi hizi za ushairi yameanza kupokelewa kuanzia tarehe 15 Februari 2022. Mwisho wa kutuma mawasilisho hayo ni tarehe 15 Julai 2022.

Washindi watatu katika kila lugha watatangazwa tarehe 21 Septemba 2022

Mashairi ya lugha ya Kiswahili yatapokelewa kupitia baruapepe ya mkurugenzi wa mashindano haya kwa lugha za kiafrika ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Pan-African Writers Association (PAWA), Dkt. Wale Okediran. waleokediran@yahoo.co.uk

Kwa maelezo zaidi fuatilia kupitia uzi huu;

https://www.iflacworld.org/affiliated-poetry-contest

Categorized in: