Mwaka Jana tulishuhudia ongezeko la utovu wa nidhamu shuleni.Haswa shule ziliteketezwa pasi na kujali madhara yake.Ni kutokana na swala hili waziri wa Elimu Prof.George Magoha aliponena kuwa adhabu ya fimbo ni lazima kama ibada irudishwe shuleni kama awali. Nidhamu huchangia pakubwa katika Elimu ya wanagenzi. Swala hili lingali linaning’inia hewani kwani hatua husika hazijatekelezwa na washika dau wote katika idara ya Elimu. Ni ombi langu,Waziri wa Elimu atabuni jopo maalum litakalolivalia njuga swala hili ili kupata suluhu.Ikiwa watangoja,ngoja ngoja hiyo itaumiza matumbo na huenda visa vya utovu wa nidhamu shuleni vikaongeza maradufu. Tusipoziba ufa,tutajenga ukuta na kidole Cha lawama kitaelekezwa Kwa idara husika na jamii Kwa kutowajibika..!!
Martin Mwendwa Mwanthi, Tubonge Youth initiative-Likoni,Mombasa.
WRITER – MARTIN
