Ungamuona dhahiri, kidari akitanua
Asema kama amiri,kwa nguvu akipumua
Mwenzangu usifikiri,dhiki yuazitatua
Ufisadi ni hatari,hatari kuliko nyoka
Fikiri nakusaili,ndugu yangu mzalendo
Jinsi ya kuukabili,ukongo wenye uvundo
Lisije tutia feli,dhiki na nyingine kondo
Ufisadi ni hatari,hatari kuliko bafe
Sasa tushike hatamu,taifa kulikomboa
Wakenya tutakadamu,hizi taka kuzizoa
Haramu iwe haramu,tusibakishe madoa
Ufisadi ni hatari, hatari kuliko swila
Dibaji siiandiki,akili yangu mauza
Ila ndugu wastahiki,tusisite kuliwaza
Ufisadi ni tariki,iliyofunika kiza
Ufisadi ni hatari,kuliko mtambaachi
Moses Chesire
Sumu ya waridi
Kitale
WRITER – MOSES
